Header Ads

Breaking News

KARIBU SHULE YA MSINGI SOKON ONE

Habari mpendwa!
Karibu sana katika blogu ya Shule ya Msingi Sokon One iliyopo kata ya Sokon I ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha!
Shule ya Sokon One ni shule ya uma inayomilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohudumia wanafunzi kutoka  maeneo ya karibu na shule hii kama vile Jr, Field Force, Morombo, Ngusero na Sombetini.
Blogu hii imeandaliwa maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya masomo tayarishi kwa ajili ya kujiunga na Elimu ya Sekondari kwa wanafunzi mbalimbali katika Kata ya Sokon One hususan wale waliohitimu Elimu ya Msingi katika shule hii kwa mwaka 2017.
Mazingira ya Shule ya Msingi Sokon One. Picha imepigwa na Goustone Isole- 18 Septemba, 2017
Katika blogu hii utafurahia kuona matukio mbalimbali katika habari, picha na video. Utaona mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, walimu husika wakati wa kipindi cha masomo, shughuli mbalimbali nje ya darasa. Pia ratiba ya masomo kipindi chote cha masomo na matokeo ya masomo mbalimbali!

Ni matarajio yetu wanafunzi watafurahia blogu hii kwa kumbukumbu za baadae! Wanafunzi bora wataonekana katika kurasa zao maalum pamoja na marafiki zao!

Karibuni sana!
Goustone Isole

No comments